1 Chronicles 22:1-6

1 aNdipo Daudi akasema, “Nyumba ya Bwana Mwenyezi Mungu itakuwa mahali hapa, pia pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Israeli.”

Maandalizi Kwa Ajili Ya Hekalu

2 bKwa hiyo Daudi akatoa amri wakusanyike wageni wote waliokuwa wanaishi Israeli, na kutoka miongoni mwao akaweka waashi ili kuchonga mawe kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mungu. 3 cDaudi akatoa chuma tele ili kutengenezea misumari kwa ajili ya mafungo ya malango ya nyumba na shaba tele isiyopimika. 4 dPia akatoa magogo ya mierezi yasiyohesabika, kwa kuwa Wasidoni na Watiro walikuwa wamemletea Daudi idadi kubwa ya mierezi.

5 eDaudi akasema, “Mwanangu Sulemani bado ni mdogo wa umri na hana uzoefu. Nyumba itakayojengwa kwa ajili ya Bwana inatakiwa iwe yenye uzuri mwingi na sifa na fahari mbele ya mataifa yote. Kwa hiyo nitaifanyia matayarisho.” Daudi akafanya matayarisho makubwa kabla ya kifo chake.

6 fKisha akamwita Sulemani mwanawe akamwagiza kujenga nyumba kwa ajili ya Bwana, Mungu wa Israeli.
Copyright information for SwhKC